Balozi
wa Norway humu nchini Victor Renneberg ameyataka mashirika ya kijamii Pwani kuhakikisha yanatekeleza majukumu yao vilivyo ili kuafikia demokrasia
nchini.
Akiongea kwenye kikao na wanhabari katika ofisi za
shirika la Haki Afrika Renneberg amesema kuwa anatarajia kukutana na vikundi
vya vijana nchini ili kujali na kuzungumzia changamoto zinazowakabili
Kwa upande wake mwenyekiti wa Haki Afrika Hussein
Khalid amesema kuwa anatarajia ushirikiano mwema baina ya Kenya na Norway
ambapo pia ameyataka mataifa mengine ya kigeni kutalii eneo hili ili kujionea
hali ilivyo.
Renneberg na kikosi chake anatarajiwa kukutana na
gavana wa Mombasa Ali Hassan na seneta Hassan Omar hii leo kabla ya kukutana na
maafisa wakuu wa polisi katika kaunti ya Mombasa.
No comments:
Post a Comment
COMMENT