Nchini Mali, watu 600 wako chini ya uchunguzi wa maambukizi ya Ebola wakati huu nchi hiyo ya Afrika Magharibi ikiweka mikakati kuzuia maambukizi mapya ya ugonjwa huo hatari.
Wakati hayo yajikiri, viongozi wa serikali walikutana
Jumatatu Novemba 17 kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa usalama unaimarishwa
hasa katika mpaka wake na Guinea, nchi iliyoathiriwa zaidi na ugonjwa wa Ebola.
Hadi sasa watu wawili wamepoteza maisha nchini Mali
baada ya kuambukizwa Ebola.
Rais Ibrahim Boubacar Keita, amezuru katika mpaka wa
nchi hiyo na Guinea katika eneo la Kouremale na kutoa wito kwa wenyeji
kuhakikisha kuwa wanasaidia kupambana na ugonjwa huu kwa kutoa ripoti kwa
yeyote anayeshukiwa kuambukizwa.
Umoja wa Ulaya umeahidi kutoa Dola Milioni 15 kwa nchi
ya Mali, Senegal na Cote d'Ivoire ili kuweka mikakti ya kuzuia kusambaa kwa
Ebola kutoka nchi jirani kama Guinea, Liberia na Siera Leone.
Shirika la afya duniani, limesema zaidi ya watu elfu
tano wamepoteza maisha katika nchi za Afrika Magharibi kutokana na ugonjwa wa
Ebola.