Friday 17 October 2014

CHAMA CHA MIKOPO YA BODABODA CHAZINDULIWA KILIFI



Chama kitakachowasaidia waendeshaji wa bodaboda kuchukua mikopo kimezinduliwa katika kaunti ya Kilifi.

Akiwahutubia waendeshaji hao katika jumba la Juwaba  Seneta mteule Mvita Kisasa amewataka wajisajili kwa vyama hivyo kwa minajili ya kuendeleza biashara zao.

Vilevile Kisasa ameeleza kuwa sababu ya kuzindua chama hicho ni kuifufua sekta hiyo ya uchukuzi inayokumbwa na changamoto nyingi. 

Mkutano huo ulihudhuriwa na mkuu wa polisi kaunti hiyo Justine  Nyaga.

No comments:

Post a Comment

COMMENT