Wednesday 25 March 2015

NATAKA KUWA KARIBU NA MWANANGU ASEMA CHRIS BROWN

Ni kawaida kwa watu mashuhuri kuwaruka mpango wa kando pale wanapopata mimba na hatimaye kuzaa mtoto. Lakini mambo ni tofauti kwa mwimbaji wa nyimbo za RnB, Chris Brown.

Kulingana na vyanzo vya kuaminika Brown anapangia kumhamisha Nia Guzman, mwanamitindo aliyezaa naye mtoto Royal, kutoka anakoishi hadi sehemu ya karibu na kwa Brown.

Chris anayeishi L.A anataka kuwa karibu na motto wake na angependa kumwona kila siku na ndio maana anamtaka Nia kuhamia L.A.

Hata hivyo Nia na Brown hawajapatana kuhusu ulezi wa motto huyo. Inasemekana Brown hupeana pesa nyingi kupita kiasi kinachohitajika kwa malezi ya Royal. Jambo linalomkera Nia na kwa sasa anapania kwenda mahakamani ili Brown apunguze ngwenje anazopeana kwa ajili ya malezi ya Royal.

Tuesday 24 March 2015

DEDE RECORDS FOUNDER GETS A CHILD

Dede records owner Sammy Gitonga is now a proud dad to a baby girl.

"Baby Shiku Gitonga, just born.. 3.9 kgs! Thank you God for the blessings."
Wrote the music doctor on his official facebook account accompanied by a picture of his angel.
Congratulation Sammy Gitonga!

SENETA AVALIA MAVAZI YA KIMIJIKENDA KWENYE KONGAMANO LA KIMATAIFA

Baada ya kuwarai wanawake wakipwani hususan wa jamii ya wamijikenda kuvalia nguo za kitamaduni almaarufu mahando kama njia mojawapo ya kuwavutia watalii, Seneta mteuliwa wa Mombasa, Emma Mbura ameamua kuwa katika mstari wa mbele katika jambo hilo.

Seneta huyo aliamua kutupilia mbali matamshi yaliyopinga ushauri wake na kuvalia nguo za kitamaduni alipokuwa akihudhuria kongamano la wanawake linalofanyika Uhabeshi (Ethiopia) kama njia moja ya kuuza utamaduni wa kipwani.
Seneta huyo alitundika picha mtandaoni zilizo ambatanishwa na msemo "my culture my identity"


PICHA : SUSUMILA ASHOOT VIDEO YA KIDEDE

Msanii mkali wa  pwani susumila atakuwa akiachilia video ya wimbo kidede aliyomshirikisha Dazla hivi karibuni.

Kupitia picha alizozitundika mtandaoni, Susumila alielezea furaha yake ya kuweza kukamilisha shooting ya video hiyo pasipo tashwishwi yeyote ile.






ANGELINA JOLIE ATOA KIZAZI CHAKE

Muigizaji maarufu Angelina Jolie amefanyiwa upasuaji wa kukitoa kizazi chake kama njia ya kuzuia saratani mwilini mwake.

Jolie ambaye alimpoteza mamake na nyayake kwa ugonjwa wa saratani aliliandikia gazeti la NY Times akielezea kwa nini alichukua hatua hiyo.
 Kulingana na daktari wa Jolie, alipatikana na chembe chembe zinazoweza kusababisha saratani majuma mawili yaliyopita.
 Uchunguzi wa daktari ulionyesha kulikuwa na uwezekano wa asilimia 87 ya kupata saratani ya matiti na asilimia 50 ya kupata saratani ya njia ya uzazi.
 Angelina amekuwa akijitayarisha kupigana na saratani kwa miaka miwili sasa baada ya kufanyiwa “mastectomy” miaka miwili.
 Kwa sasa Jolie anasema ameingia menopause ya kulazimishwa. Hata hivyo bado anajihisi kama mwanamke kamili "I feel feminine, and grounded in the choices I am making for myself and my family. l know my children will never have to say, 'Mom died of ovarian cancer.'"