Baada ya kuwarai wanawake wakipwani hususan wa jamii ya wamijikenda kuvalia nguo za kitamaduni almaarufu mahando kama njia mojawapo ya kuwavutia watalii, Seneta mteuliwa wa Mombasa, Emma Mbura ameamua kuwa katika mstari wa mbele katika jambo hilo.
Seneta huyo aliamua kutupilia mbali matamshi yaliyopinga ushauri wake na kuvalia nguo za kitamaduni alipokuwa akihudhuria kongamano la wanawake linalofanyika Uhabeshi (Ethiopia) kama njia moja ya kuuza utamaduni wa kipwani.
Seneta huyo alitundika picha mtandaoni zilizo ambatanishwa na msemo "my culture my identity"
No comments:
Post a Comment
COMMENT