Familia iliyopoteza mtoto wa mwaka mmoja baada ya mtoto huyo kuvamiwa na kutafunwa na mbwa, imelipwa fidia ya shilling laki moja.
Kulingana na ripoti ya
gazeti la “Daily Nation” fidia hiyo iliafikiwa baada ya mwenye mbwa huyo, Bwana
Mohamed Hajj Awadh, ambaye pia nimwenye shamba la “kilifi’s shariani poultry
farm”, kujadiliana na wazazi wa mwendazake.
Mtoto huyo alivamiwa
pale alipokuwa akitambaa kumfuata babake aliyekuwa akielekea shambani mwa bwana
Mohamed anamo fanya kazi kama kibarua.
Alipokuwa akithibitisha
kupokea kwa fidia hiyo, baba ya mtoto huyo, Mwampa kadodo, mwenye umri wa miaka
27, alisema kwamba yeye na mkewe walitaka kuendeleza uhusiano mwema na mwajiri
wake.
Ijapo kuwa uchungu wa
kumpoteza mwana ulikuwa mwingi, ametambua kwamba hakuna anachoweza kukifanya ili kumrudishia
mwanawe uhai.
“ Ni uchungu ndio
lakini kwa upande mwingine huu ulikuwa mpango wa mungu ambao hatuna nguvu
kuuliko. Uhusiano wetu na mwajiri wangu bado ni mzuri nab ado nafanya kazi
shambani mwake.”
Mwenye shamba pia
alikuwa na huzuni moyoni kuhususiana na kisa chote.
“ilikuwa jambo la
kushtua na kuhuzunisha,” alisema.
Bwana Kadodo, baba ya
watoto watano, wavulana watatu na wasichana wawili alisema kwamba atatumia
fidia hiyo kuwasomeshea watoto wake walio na umri kati ya mmoja na sita.
“Msichana wangu wa
kwanza yuko darasa la kwanza kama mdogo wake. Nitazitumia pesa hizi kulipia
karo yao. Hawa wengine watatu bado wako nyumbani,” Alisema.
Mapatano hayo yaliiafikiwa
chini ya uelekezi wa afisaa kutoka kwa shirika la haki za kibinadamu, Eric
Mgoja. Mgoja alizisifu pande zote mbili kwa hatua walioichukua ili kuona kwamba
utata baina yao umetatuliwa.
Hata hivyo mama ya
mtoto huyo amelihama shamba hilo
kutokana na majeraha ya kisaikolojia.
No comments:
Post a Comment
COMMENT