Saturday 12 April 2014

TEACHER WANJIKU AZIDI KUTAPATAPA



Mchekeshaji na mwanaburudani almarufu teacher wanjiku amejipata tena matatani.
Mchekeshaji huyo ambaye kipindi chake kilisitishwa baada ya kwenda hewani kwa mara ya kwanza na runinga moja nchini Kenya, kwa kutofanya vyema. Inasemekana alitaka kurudi katika Kampuni ya laugh industry inayo ongozwa na mchekeshaji Daniel Ndambuki almarufu churchhill. Kampuni aliyotengana nayo ili kuanzisha kipindi chake ambacho hakikuvutia mashabiki wengi.
Ni hatua hii ambayo imemtamausha kwani churchhill, aliye itambua talanta ya teacher wanjiku, hayuko tayari kumpa nafasi tena. 

Kulingana na duru za kuaminika “laugh industry” iko katika harakati za kupunguza gharama na hivyo basi haina dhamira ya kujiongezea gharama zisizokuwa na manufaa.
Inaaminika wawili hao hawakupatana kwa kile kinachosemekana kuwa Teacher Wanjiku alitaka mengi, ambayo kampuni ya laugh industry haiko tayari kumtimizia.
Kwa sasa kampuni ya laugh industry imewaachishakazi wafanyikazi 50 ili kuboresha vipindi vyao: churchhill show na churchhill raw.
Twamtakia kila la heri!
#Kulingana_ na_ gazeti_ la_ standard

No comments:

Post a Comment

COMMENT