Muigizaji maarufu Angelina Jolie amefanyiwa upasuaji wa kukitoa kizazi chake kama njia ya kuzuia saratani mwilini mwake.
Jolie ambaye alimpoteza mamake na nyayake kwa ugonjwa wa saratani aliliandikia gazeti la NY Times akielezea kwa nini alichukua hatua hiyo.
Kulingana na daktari wa Jolie, alipatikana na chembe chembe zinazoweza kusababisha saratani majuma mawili yaliyopita.
Uchunguzi wa daktari ulionyesha kulikuwa na uwezekano wa asilimia 87 ya kupata saratani ya matiti na asilimia 50 ya kupata saratani ya njia ya uzazi.
Angelina amekuwa akijitayarisha kupigana na saratani kwa miaka miwili sasa baada ya kufanyiwa “mastectomy” miaka miwili.
Kwa sasa Jolie anasema ameingia menopause ya kulazimishwa. Hata hivyo bado anajihisi kama mwanamke kamili "I feel feminine, and grounded in the choices I am making for myself and my family. l know my children will never have to say, 'Mom died of ovarian cancer.'"
No comments:
Post a Comment
COMMENT