Wednesday 25 March 2015

NATAKA KUWA KARIBU NA MWANANGU ASEMA CHRIS BROWN

Ni kawaida kwa watu mashuhuri kuwaruka mpango wa kando pale wanapopata mimba na hatimaye kuzaa mtoto. Lakini mambo ni tofauti kwa mwimbaji wa nyimbo za RnB, Chris Brown.

Kulingana na vyanzo vya kuaminika Brown anapangia kumhamisha Nia Guzman, mwanamitindo aliyezaa naye mtoto Royal, kutoka anakoishi hadi sehemu ya karibu na kwa Brown.

Chris anayeishi L.A anataka kuwa karibu na motto wake na angependa kumwona kila siku na ndio maana anamtaka Nia kuhamia L.A.

Hata hivyo Nia na Brown hawajapatana kuhusu ulezi wa motto huyo. Inasemekana Brown hupeana pesa nyingi kupita kiasi kinachohitajika kwa malezi ya Royal. Jambo linalomkera Nia na kwa sasa anapania kwenda mahakamani ili Brown apunguze ngwenje anazopeana kwa ajili ya malezi ya Royal.

No comments:

Post a Comment

COMMENT