Friday 26 June 2015

CELEBRITY NEWS: SUSUMILA AFICHUA SABABU YA KUFUNIKA MANENGUO KWENYE VIDEO YA WIMBO IHALE

SUSUMILA. PHOTO||COURTESY
Ni kawaida kwa wanamuziki hapa nchini na ulimwengu mzima kwa ujumla, kuwatumia vibaya wasichana  katika video za nyimbo pasipokujali ni nani atakayezitazama.

Wengi wao hunengua viuno huku wakiwa nusu uchi. Jambo ambalo wapenzi wa mziki wa kizazi kipya hulishabikia kwa sana, lakini mambo ni tofauti ikiwa video ya Susumila alioiachilia hivi majuzi ni ya kuzingatiwa. Kwani ni video a kupigiwa mfano, na ya aina yake.

Kinyume na wasanii wengine susumila, mwanamziki kutoka ukanda wa pwani ya Kenya, aliamua kutumia vijibango hai kufunika manenguo ya dada mmoja katika video yake. Ni jambo liloshangaza wengi, lakini kulingana na Susumila, kuna sababu mwafaka kwa nini akafanya hivyo.

nimefunika kwa sababu najua mziki wangu unashabikiwa na watu wakila umri, kwa hivo nisingetaka kuwakwaza mashabiki wangu pengine waone haya kuangalia video ile mbele ya familia zao.” Alisema Susumila

 Kando na hayo, Susumila kwa sasa anayetamba na vibao kidekide na Ihale, amekuwa akifanya mziki wa mtindo tofauti na ule wa pwani.  Ni hatua hii ya kufanya mitindo ya mziki tofauti na ule wa pwani uliopelekea wengi kusema kwamba amepoteza dira na ameanza kuiga.

Lakini kulingana na Susumila sio ati anaiga bali upana wa mtandao wa mashabiki wake ndio uliochangia pakubwa kwa yeye kufanya mitindo tofauti ya mziki.


“siezi sema naiga kwa sababu music is universal na siimbii maahabiki wapwani pekee that is why leo utaona nimefanya afrobeat mara kesho lingala mara wakati mwengine hiphop au reggae mimi hua sijekei limit katika kutayarisha mziki wangu” alisema Susumila.

No comments:

Post a Comment

COMMENT