Ukeketaji wa wasichana unaoendelea kutekelezwa kila uchao katika jamii ya Boni kaunti ya Lamu umetajwa kama changamoto kuu inayosababisha kudorora kwa viwango vya elimu katika eneo hilo.
Haya ni kwa mujibu wa afisa mkuu wa
elimu ya afya,jinsia na jamii katika kaunti hiyo Hamisi Kaviha ambapo amesema
hali hiyo inaendelea kuzidi na kusababisha wasichana wengi kupachikwa mimba
miongoni mwao 15 kutoka shule ya msingi ya Bargoni.
Akizungumza na wanahabari wakati wa
ziara yake katika eneo la Boni Kaviha ameeleza kuwa afisi yake ilibaini kwamba
shughuli hiyo hutekelezwa kwa watoto walio kati ya umri wa miaka 9 na 10 hasa
kwenye sherehe za mwezi December.
Amedokeza kuwa baada ya wasichana hao
kukeketwa wao hujihisi kwamba wako katika nafasi ya kupata kuolewa mapema kabla
ya umri wao kufika.
Hata hivyo amesema wameweka mikakati ya
kushirikiana na machifu pamoja na viongozi wengine ili kuwakamata wale ambao
wanahusika na maafa hayo.
No comments:
Post a Comment
COMMENT