Wednesday 13 August 2014

TAWI LA KEFORA LAOMBOLEZA KIFO CHA REFEREE AKOKO:

Aliyekuwa referee wa ligi kuu nchini KPL Adel Akoko , amefariki.
Kulingana na familia ya marehemu, mwendazake aliaga dunia mwendo wa saa kumi alasiri ya jana kwenye hospitali kuu ya mkoa wa pwani alikolazwa baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Kufuatia kifo chake, meneja wa marefarii tawi la kusini mwa pwani Kennedy Kiema pamoja na mwenyekiti wa marefarii ukanda wa pwani Bw. Shilingi fumbwe wametoa risala zao za rambi rambi kwa jamaa na marafiki.
Hadi mauti yake, Adel alikuwa katibu wa chama cha mareferee tawi la kusini mwa pwani.

No comments:

Post a Comment

COMMENT